Shirika la habari AhlulBaya (a.s) ABNA: viongozi wa mkoa wa Anbar nchini Iraq siku ya Jumamosi wametangaza kuwa majeshi yanayo pambana dhidi ya magaidi nchini Iraq yamefanikiwa kukomboa sehemu mbili nyingine pia kuyakomboa makao makuu ya jeshi la Polisi katika wilaya ya Hit iliopo katika mkoa wa Anbar, ambapo hivi sasa kamili mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
“Malu Allah Al Saidi” mkuu wa wilaya ya Baghdadi katika mkoa wa Ambar ameongeza kusema kuwa: majeshi ya Iraq yamewiza kukomboa miji miwili mipya ambayo ni ya “Sakak” na “Askariy” katika wilaya ya Hit.
Aidha ameongeza kusema kuwa majeshi ya Iraq yanaendeleza mashambulizi yake kwa lengo la kuikomboa kamili wilaya hiyo kutoka mikononi mwa vikundi vya kigaidi vya Daesh.
Kadhalika amesema mwendelezo wa kuikomboa wilaya hiyo umekuwa na uzito kwa kiasi chake kutokana na kuwepo na mitego ya mabomu iliotekwa katika sehemu hiyo kitu ambacho kinaifanya harakati za kuikomboa ehemu hiyo inakuwa na uzito.
Wilaya ya Hit inaumbali wa kilometa 70 mpaka kufika mashariki mwa wilaya ya Ramad iliopo katika mkoa wa Anbar amapo katikati ya mwaka 2014 wilaya hiyo iliingia mikoni mwa kikundi cha kigaidi.
Kamanda mkuu wa mashambulizi dhidi ya vikundi vya kigaidi katika mkoa wa Ambari ametangaza kuwa siku ya Alhamisi iliopita ndio siku yalioanza mashambulizi maalumu kwaajili ya kuikomboa wilaya ya Hit kaskazini mwa magharibi mwa Ramadi nchini Iraq.
Mapambano ya Iraq dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh ni bado yenye kuendelea amapo mpaka sasa majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuikomboa wilaya ya Ramadi ilipo katika mkoa wa Ambar na maeneo mingine yaliopo kaskazini mwa Iraq kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
mwisho wa Habari/290